history of miss tanzania contestants

CLick here to advertise

1994: Mrembo Aina Linda W. Maeda

Mara baada ya kushinda taji hilo na kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii, alipata ofa mbalimbali za kufanya kazi za mitindo nchini Afrika ya Kusini, na hatimaye kuhamia huko na kuishi huko kwa karibu miaka 10 ambapo aliweza kupata marafiki wa jinsia mbalimbali na kutokana na marafiki hao aliweza kupata mchumba Bwana Jean P. Guyeu, raia wa Ufaransa aliyekuwa akifanya kazi zake nchini Afrika ya Kusini. Mrembo huyo akiwa na mchumba wake huyo hatimaye walikuja nyumbani nchini Tanzania kufunga ndoa ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania . Kamati inayoendesha Mashindano ya urembo nchini iliyomuwezesha kumfikisha hapo alipo mrembo Aina Maeda. Kwa sasa mrembo Aina na mume wake wanaishi jijini Cape Town, Afrika ya Kusini.

1995: Mrembo Emily Adolf

Baada ya kuanzishwa kwa Mashindano ya urembo nchini mwaka 1994 yaliendelea kufanyika mfululizo na mwaka 1995 yalipanuka zaidi na kupata Wawakilishi kutoka mikoani, na Mshindi kwa mwaka 1995 alikuwa Emily Adolf mwanafunzi wa Kidato cha pili shule ya Sekondari ya Central akitokea Makao Makuu Dodoma, ushindi ambao ulileta malumbano hadi Mrembo huyo ilibidi afukuzwe shule kwa madai ya kushiriki Mashindano hayo akiwa ni mwanafunzi.

 

Wanaharakati wa kutetea Haki za Wanawake nao walikuja juu na kupinga vikali kuanzishwa kwa Mashindano hayo, huku Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA wakiwa wamelivalia njuga suala hilo , pamoja na Taasisi mbalimbali za Dini zikipinga vikali suala la warembo hao kupita jukwaani huku wakiwa wamevalia Vichupi, [swimming costume au Bikini ]

 

Baadaye mwaka huo huo Baraza la Sanaa la Taifa ilibidi kuweka Kanuni na Taratibu za kuendesha Mashindano hayo na kuzuia vazi hilo la vichupi, pamoja na wanafunzi wote wa shule za Msingi na Sekondari kutoshiriki Mashindano hayo.

 

Mrembo Emily Adolf [Pichani] aliwakilisha Nchi pia katika Mashindano ya Urembo ya Dunia na aliporejea, Kamati ya Miss Tanzania kwa kushirikiana Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete wakati huo akiwa Waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akishirikiana na Waziri wa Elimu wa wakati huo waliweza kumuombea nafasi ya kumaliza masomo yake mrembo huyo katika shule ya Sekondari ya Makongo.

 

Baadaye jamii ya Watanzania walianza kuelewa taratibu lengo na madhumuni ya Mashindano haya kwamba siyo kuwadhalilisha wasichana bali ni Mashindano ambayo yalikuwa yakiwapatia zawadi mbalimbali warembo hao ikiwa ni pamoja na ajira. Kwani wasichana wengi ambao walikuwa wakishiriki Mashindano haya pamoja na zawadi ya pesa taslimu na vitu mbalimbali pia walikuwa wakipata ajira mbalimbali kutoka kwa Wadhamini wa Mashindano hayo pamoja na wadau wengine ambao walikuwa wakiyafuatilia kwa karibu Mashindano hayo.

 

Mrembo Emily Adolf : Kwa sasa anamiliki Mgahawa mmoja hapa jijini uitwao Rumors Pub na pia ameolewa.

1996: Baada ya kupanuka kwa Mashindano ya urembo nchini, mwaka 1996 mrembo Shose Sinare alishinda taji la taifa.

Mrembo Shose Sinare alikuwa akitokea mkoa wa Arusha na aliweza kuwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini India . Mrembo Shose alikuwa mrembo wa kwanza kutoka katika nchi za Afrika aliyeweza kuitisha mkutano na Waandishi wa Habari wa kimataifa wakati wa shindano hilo la urembo la dunia na kuelezea jinsi washiriki kutoka nchi za Afrika walivyokuwa wakibaguliwa.

 

Baada ya kurejea nchini na kumaliza muda wake wa mwaka mmoja wa kazi za jamii, mrembo Shose Sinare alipata nafasi ya kufanya kazi za Mitindo [Modeling] nchini Italy kwa muda mrefu na hatimaye kujipatia mchumba raia wa Italy na kufunga naye ndoa.

1997: Mrembo Saida Kessy kutoka mkoa wa Arusha

1997: Warembo kutoka mikoani walionekana kushika chati, kwani mwaka uliofuata [1997] Mrembo Saida Kessy kutoka mkoa wa Arusha aliweza kushinda taji la Miss Tanzania na kuwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia. Mrembo Saida Kessy kama warembo wengine waliomtangulia hawakuweza kushika nafasi yeyote ya juu, na aliporudi nchini aliendelea kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja akiwa kama mrembo wa taifa, na pia aliweza kupata ofa mbalimbali za kazi ya uanamitindo.

 

Mrembo Saida Kessy aliyezaliwa mwaka 1975 kwa sasa anafanya kazi katika Mahakama ya Kimataifa ICTR iliyopo Arusha, ameolewa na pia ana mtoto mmoja.

 

1998: Mrembo Basila Mwanukuzi Mrembo kutoka Wilaya ya Kinondoni

1998: Mwaka huu ilikuwa ni zamu ya warembo kutoka mkoa wa D'salaam kwani waliweza kushika nafasi zote tatu za juu. Mrembo Basila Mwanukuzi Mrembo kutoka Wilaya ya Kinondoni, ndiye aliyeshinda taji la Miss Tanzania akifuatiwa na mrembo Nuru Doto Butamu pamoja na Diana Muhere.

 

Mrembo Basila Mwanukuzi aliyezaliwa tarehe14/6/1978 .. pia aliweza kuwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia. Aliporejea na kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii aliweza kupata ofa mbalimbali za kazi za Mitindo nchini Marekani ambapo aliishi huko kwa muda na kurejea nchini na kufanya kazi na Kampuni ya Multichoice, na baadaye kuajiriwa na Shirika la Umoja na Mataifa. Mrembo Basila Mwanukuzi, amefanya kazi na UNDP jijini Pretoria Afrika ya Kusini, na baadaye alihamia Addiss Ababa Ethiopia , kwa sasa yupo jijini D'salaam akiendesha biashara yake binafsi ijulikanalo kama The Look Beauty Parlor [Unisex]

1999: Mrembo Hoyce Temu

1999: Mrembo Hoyce Temu aliyezaliwa tarehe 20 Machi 1978 akitokea Wilaya ya Ilala jijini D'salaam ndiye aliyeshinda taji la Miss Tanzania na kuwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini Uingereza mwaka huo. Mrembo Hoyce Temu anajulikana zaidi kama Mrembo wa Karne, hasa ushindi wake ulikuja wakati dunia ikitoka karne ya 20 na kuingia karne ya 21. Mrembo Hoyce Temu ambaye alifahamika zaidi kama Mrembo wa Millenium.

“ Miss Millennium 1999” ni mrembo aliyeiletea sifa sana Kamati ya Miss Tanzania na nchi kwa ujumla kwa kufanya kazi nyingi za jamii hata alipomaliza muda wake wa mwaka mmoja, mrembo Hoyce Temu ameendelea kufanya kazi za jamii hadi hivi sasa kwa kutumia jina la Miss Tanzania 1999.

 

Mrembo Hoyce Temu pamoja na kazi mbalimbali za Mitindo alizokuwa akizifanya pia alifanya kazi ya kuhamasisha kuchangia mfuko wa chakula kwa nchi maskini uliokuwa ukijulikana kama WFP Telefood. Baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa shughuli za jamii Mrembo Hoyce Temu alihamia nchini Marekani ambapo pamoja na shughuli zingine alizokuwa akizifanya pia alikuwa akisomea Shahada ya Juu ya Sheria katika Chuo cha Ohio nchini Marekani.

 

Kwa sasa yupo nchini akifanya shughuli binafsi za Ushauri [Consultancy]

2000: mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kutoka Wilaya ya Ilala

2000: Warembo wa jiji la D'Salaam waliendelea kushinda Taji la Miss Tanzania na mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kutoka Wilaya ya Ilala ndiye aliyeshinda taji la Mrembo wa Taifa kwa mwaka huo. Mrembo Jacqueline Ntuyabaliwe kama ilivyokuwa kwa warembo wengine aliwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia na aliporejea aliendelea kulitumikia taifa kwa kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

Mrembo Jacqueline aliyezaliwa tarehe 6 Desemba 1978 kabla ya kushiriki Mashindano ya urembo alikuwa ni msanii wa muziki ambaye alikuwa akiimba na bendi iliyokuwa ikijulikana kama The Tanzanite. Kushinda kwake taji la Miss Tanzania kulimuongezea Hadhi na jina lake kufahamika zaidi na hatimaye kuendeleza fani yake ya muziki kama Msanii wa Bongo Fleva anayejitegemea. Hadi sasa hivi ameshatoa albamu kadhaa na pia amekuwa akitumbuiza katika maonyesho mbalimbali na katika Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania .

2001: Mrembo Happiness Magese

2001: Kama kuna mwaka ambao kidogo mrembo wa Taifa Miss Tanzania aliweza kutingisha katika Mashindano ya urembo ya dunia ulikuwa mwaka 2001 ambapo Mrembo Happiness Magese akitokea Wilaya ya Temeke alishinda Taji la Miss Tanzania na kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya urembo ya dunia yaliyofanyika nchini Afrika ya Kusini mwaka huo.

 

Mrembo Happiness Magese mwenye vipimo vya urefu 5'79” alikuwa ni mrembo aliyetingisha warembo wote waliotokea bara la Afrika, na hata Mrembo wa dunia aliyeshinda katika mwaka huo Mnigeria Agbani Darego alikiri mbele ya Vyombo vya Habari kwamba mrembo Happiness Magese kutoka Tanzania ndiye aliyekuwa tishio kwake.

 

Mrembo Happiness Magese aliyezaliwa tarehe 22 Septemba 1982 mara baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii hakukaa nchini alichukuliwa na Kampuni ya Elite Fashions inayofanya kazi za Mitindo huko Afrika ya Kusini na kuzunguka nchi mbalimbali akifanya kazi mbalimbali za mitindo. Hadi hivi mrembo huyo bado yupo nchini huko kwa shughuli hizo.

2002: Mrembo Angela Damas

2002: Warembo wa Jiji la D'salaam waliendelea kushika chati kwa kutwaa Taji la Miss Tanzania , Mrembo Angela Damas kutoka Wilaya ya Ilala aliweza kushinda taji la Mrembo wa Taifa kwa mwaka 2002. Mrembo Angela Damas aliyezaliwa tarehe

16 Februari 1982. kama ilivyo kwa warembo wengine, aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya Dunia ambayo kwa mwaka huo yalikuwa yafanyike barani Afrika nchini Nigeria lakini kutokana na sababu za kisiasa yalihamishiwa nchini Uingereza.

 

Mrembo Angela Damas baada ya kumaliza mwaka wake mmoja wa kazi za jamii, alifanya kazi katika Mashirika mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na Kampuni ya simu za mkononi ya Mobitel [Buzz] kama Meneja Masoko. Kwa sasa mrembo Angela Damas yupo nje ya nchi akifanya kazi na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa. [UNDP]

2003: mrembo Sylivia Bahame kutoka Wilaya ya Temeke

2003: Warembo wa Jiji la D'salaam walikuwa wakibadilishana Taji la Miss Tanzania kutoka Wilaya ya Ilala mwaka 2002, Taji la Miss Tanzania 2003 lilinyakuliwa na mrembo Sylivia Bahame kutoka Wilaya ya Temeke. Na kama ilivyo ada mrembo Sylivia Bahame aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia ambayo yalifanyika Sanya China .

 

Mrembo Sylivia Bahame aliyezaliwa tarehe 5 Juni 1983 baada ya kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii, alirudi Chuo Kikuu cha D'salaam kuendelea na masomo yake ya Sheria, ambapo kwa sasa amemaliza na anafanya kazi kama Mwanasheria wa kujitegemea pia ameahidi kuwasaidia sana wanawake na wasichana warembo ambao watakuwa na matatizo mbalimbali.

2004: mrembo Faraja Kotta kutoka Wilaya ya Kinondoni

Mwaka 2004 taji la Miss Tanzania lilihama kutoka Wilaya ya Temeke na kuchukuliwa na mrembo Faraja Kotta kutoka Wilaya ya Kinondoni. Mrembo Faraja Kotta aliweza kuonyesha kipaji chake tangu mwanzo aliponyakua taji la mrembo wa Kitongoji cha Ubungo, [Miss Ubungo] na baadaye kunyakua taji la Miss Kinondoni na hatimaye kuwa Miss Tanzania .

 

Faraja Kotta aliyezaliwa tarehe 6 Mei 1985 alikuwa na kila sababu ya kufurahia ushindi wake kwani ni katika kipindi hicho hicho alichoshinda taji la Miss Tanzania, alitangazwa kuwa Mwanafunzi bora wa kike wa mwaka 2004 kwa kuweza kushika nafasi ya juu, [Top 5] katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha sita.

 

Mrembo Faraja Kotta aliwakilisha nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia ambayo kwa mara ya pili mfululizo yalifanyika tena Sanya nchini China .

 

Mrembo Faraja Kotta baada ya kurejea nchini na kumaliza mwaka mmoja wa kazi za jamii alijiunga na Chuo Kikuu cha D'salaam ambapo anachukua masomo ya Sheria hadi hivi sasa.

2005: Miss Tanzania Nancy Sumari

 

2005: Katika miaka 10 ya mwanzo ya Mashindano haya toka mwaka 1994 hadi 2004 yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara huku Warembo wa Taifa wakijitahidi kufurukuta na kufanya vizuri ili kuibuka washindi katika Mashindano ya Urembo ya Dunia lakini waliambulia patupu hadi mwaka 2005 Miss Tanzania Nancy Sumari aliweka Historia ya Dunia kwa kunyakua Taji la Mrembo wa Dunia, Kanda ya Afrika. [Miss World Africa]

 

Ushindi ambao uliwafurahisha takribani Watanzania wote na kupokelewa na mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, na baadaye kufanyiwa Tafrija kubwa ndani ya viwanja vya Ikulu.

 

Nyota ya Mrembo Nancy Sumari ilianza kung'ara tangu hapa Nchini baada ya kushinda Taji la Mrembo wa kitongoji cha Dar Indian Ocean mshindi wa pili nyuma ya mrembo Natalia Noel. Hata hivyo Mrembo Nancy Sumari hakukata tamaa alijifua zaidi na katika shindano la urembo la Kanda ya Kinondoni Mrembo Nancy Sumari aliweza kunyakua taji la Miss Kinondoni akimuacha mrembo Natalia Noel nyuma yake.

[ + ] read more

2006: WEMA SEPETU

2006: WEMA SEPETU : Mrembo wa kwanza wa Taji la REDD'S Miss Tanzania , ni mrembo mwenye kipaji cha uigizaji na kwa sasa anavuma zaidi katika Filamu za Kitanzania.

 

 

 

 

 

 

2007: RICHA ADHIA

2007: RICHA ADHIA: Mrembo wa pili wa Taji la REDD'S Miss Tanzania , siku zote amekuwa mkereketwa wa kuanzisha Shule / Chuo cha masuala ya urembo, na kwa sasa amefungua Clinic yake ya masuala ya urembo ijulikanayo Beauty Clinic maeneo ya Mikocheni.

 

 

 

 

2008: NASREEN KARIM Mrembo

2008: NASREEN KARIM Mrembo wa tatu wa Taji la REDD'S Miss Tanzania, ni mrembo aliyemaliza elimu ya Kidato cha 6 na kwa sasa anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu kwa ajili ya masomo ya Juu.

 

 

 

 

 

2009: NASREEN KARIM Mrembo

2009: NASREEN KARIM Mrembo wa tatu wa Taji la REDD'S Miss Tanzania, ni mrembo aliyemaliza elimu ya Kidato cha 6 na kwa sasa anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu kwa ajili ya masomo ya Juu.

 

 

 

 

 

2010 : NASREEN KARIM Mrembo

2010 : NASREEN KARIM Mrembo wa tatu wa Taji la REDD'S Miss Tanzania, ni mrembo aliyemaliza elimu ya Kidato cha 6 na kwa sasa anatarajia kujiunga na Chuo Kikuu kwa ajili ya masomo ya Juu.

Gallery

[Pichani] ambaye ameolewa hivi karibuni jijini D'salaam, tarehe 30 Desemba 2006,

 

Mrembo Shose Sinare. [Pichani wa kwanza kulia] kwa sasa anafanyakazi kama Meneja katika Benki ya Stanbic jijini D'salaam, ameolewa na ana watoto wawili.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mrembo Faraja Kotta kwa msaada kutoka Taasisi ya Youth Net inayofadhiliwa na USAID ameweza kutunga kitabu alichokiita “Faraja ya Usichana” ambacho kinatolewa bure kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Matarajio ya Mrembo Faraja Kotta ni kuwa Balozi atakayeiwakilisha Tanzania nje ya nchi.

 

 

 

 

[Mrembo Nancy Sumari [kulia] akiwa na mshindi wa pili Natalia Noel]